http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

samatta azidi kuwwika africa


CAF KOMBE la SHIRIKISHO: SAMATTA APIGA BAO, MUCULMANA HOI!

MBWANA_SAMATTA_IN_TP
Katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mchujo ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho, Supastraika wa Tanzania, Mbwana Samataa, alifunga Bao na kuisaidia TP Mazembe kuisambaratisha Liga Muculmana de Maputo kwa Bao 4-0 katika Mechi iliyochezwa huko Lubumbashi.
Raundi hii imezikutanisha Timu 8 zilizotolewa Raund ya Pili ya CAF CHAMPIONZ LIGI na zile zilizoshinda Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho.
TP Mazembe ilibwagwa nje ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Orlando Pirates ya Afrika Kusini baada ya kufungwa Bao 3-1 huko Afrika Kusini na wao kushinda 1-0 waliporudiana Mjini Lubumbashi katika Mechi ambayo walikosa nafasi nyingi za wazi za kupata Bao la pili ambalo lingewabakisha CHAMPIONZ LIGI. 
Bao za TP Mazembe:
-Dakika ya 16 Richard Kissi Boateng [Ghana]
-26 Given Singuluma [Zambia]
-53 Mbwana Samatta [Tanzania]
-80 Nathan Sinkala [Penati] [Zambia]
TP Mazembe itasafiri kwenda Maputo kurudiana na Liga Muculmana de Maputo kati ya Mei 31 na Juni 2 na Mshindi atasonga Hatua ya Makundi.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget