http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

DAVID_BECKHAM
>>BECKHAM: “NIMEBAHATIKA KUTIMIZA NDOTO YANGU!!”
>>LAMPARD: “NAMSHUKURU ABRAMOVICH KWA KUTIMIZA NDOTO YANGU!”
WAKATI Mkongwe David Beckham akitangaza kustaafu kucheza Soka mwishoni mwa Msimu huu, Mkongwe mwingine wa England, Frank Lampard, ambae jana aliisaidia Klabu yake Chelsea kuwika Ulaya na kutwaa Kombe la EUROPA LIGI, ameongezewa Mkataba wa Mwaka mmoja na Klabu yake.
DAVID BECKHAM
Baada ya kuwika katika Soka kwa Miaka 20, David Beckham, Miaka 38, ametangaza kustaafu Soka mwishoni mwa Msimu huu.
Beckham, Nahodha wa zamani wa England aliyoichezea mara 115, akiwa na Mabingwa wa England, Manchester United, aliweza kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 6 pamoja na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mwezi Januari, Beckham alisaini Mkataba wa kuichezea Paris St-Germain ya France kwa Miezi mitano.
PSG wamebakiza Mechi 2 Msimu huu, ile ya Nyumbani dhidi ya Brest Jumamosi hii na Ugenini na Lorient hapo Mei 26.
BECKHAM-Maisha ya Soka:
-1992-2003: Manchester United (Mechi 356, Magoli 85)
-1994-1995: Preston North End (Mkopo) (Mechi 5, Goli 2)
-2003-2007: Real Madrid (Mechi 157, Magoli 19)
-2007-2012: Los Angeles Galaxy (Mechi 118, Magoli 20)
-2009-2010: Mkopo AC Milan (Mechi 33, Magoli 2)
-2013: Paris St-Germain (Mechi 13)
Beckham, ambae Mshahara wake akiwa na PSG huenda kwenye Mifuko ya Hisani ya kusaidia
Watoto, ameichezea PSG Mechi 13 tangu ahamie hapo.
Akiwa na Klabu za Man United, Real Madrid, Los Angeles Galaxy, AC Milan na PSG, amefanikiwa kutwaa Makombe 19 na Ubingwa wa Ligi za  Nchi mara 10.
Beckham ametamka: “Ungeniambia nilipokuwa Mtoto kuwa ningechezea na kutwaa Mataji na Klabu niliyoipenda ya Manchested United, kuwa Nahodha wa Nchi yangu kwa fahari kubwa na kuichezea zaidi ya mara 100 na kuzichezea Klabu kubwa Duniani, ningekwambia hiyo ni ndoto!”
Aliongeza: “Nimebahatika kutimiza Ndoto hiyo!”
Beckham, aliezaliwa Mei 2, 1975, alijiunga na Man United Mwaka 1991 akiwa Mcheza Soka Mwanafunzi na kuanza kuichezea Timu ya Kwanza Mwaka 1992 na kusaini Mkataba wake wa kwanza wa Mchezaji wa Kulipwa Mwaka 1993.
Akiwa Old Trafford, Beckham alijijengea Jina kubwa Duniani kote na umaarufu wake kuongezeka pale alipomuoa Mwimbaji maarufu wa Kundi la Spice Girls, Victoria Adams.
Mwaka 2003 Beckham aliihama Man United na kwenda Spain kuichezea Real Madrid ambako alifanikiwa kutwaa Taji la La Liga Mwaka 2007 na kisha kuhamia Marekani kuichezea LA Galaxy.
Akiwa na LA Galaxy, mara mbili, Mwaka 2009 na 2010, Beckham alicheza kwa Mkopo huko Italy na Klabu ya AC Milan.
Beckham alianza kuichezea England kwenye Mechi na Moldova Mwaka 1996 na kuwa Nahodha wake kuanzia 2000 hadi 2006 na kucheza Mechi yake ya 115 na ya mwisho dhidi ya Belarus Mwaka 2009.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema: “Ni Mchezaji Bora katika maisha yake. Si hilo tu, ni Balozi Bora kwa Nchi yake!”
FRANK_LAMPARDNae Meneja wa England Roy Hodgson alitamka: "Maisha yake ya Soka yaling’ara, ni Nguli na namtakia maisha mema ya baadae!"
LAMPARD ASAINI MWAKA MMOJA CHELSEA
Frank Lampard, Miaka 34, amesaini Mkataba wa Mwaka mmoja ili kubaki Chelsea mara tu baada ya hapo jana kuisaidia kutwaa Kombe la Ulaya la EUROPA LIGI.
Akiongelea hatua hii, Lampard alisema: “Nimefurahi sana. Kila Mtu anajua nataka kuendeleza ndoto ya kubaki hapa. Namshukuru Abramovich kwa kuitimiza ndoto hii. Naipenda Klabu hii, Wafanyakazi, Wachezaji na Mashabiki!”
Wiki iliyopita, Lampard alivunja Rekodi ya Chelsea na kuwa ndie Mfungaji Bora katika Historia yao kwa kuipiku Rekodi ya Bobby Tambling ya Bao 202 kwa kufunga Bao 203.
Msimu huu, Lampard amepachika Mabao 17 ambayo ni bora tangu aifungie Chelsea Goli 27 Msimu wa 2009/10.
Lampard ameichezea Chelsea Mechi 607 tangu ahamie hapo kwa Dau la Pauni Milioni 11 Mwezi Juni 2001 kutokea West Ham.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget