http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

TRUMP KUWATIMUA WAHUNI, WAUZAJI WA MADAWA NA WAHAMIAJI ZAIDI YA MILIONI 3


 Rais Mteule wa marekani , Donald Trump ameendeleza  msimamo wake dhidi ya wahamiaji haramu nchini humo. Amedai kuwa ana mpango wa kuwafungashia virago wahamiaji haramu takriban milioni tatu,hasa wale wenye rekodi ya uhalifu.
Amesisitiza pia kuwa mpango wa kujenga ukuta upo pale pale.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu ashinde uchaguzi na kuja kuchukua kijiti cha Urais toka kwa Barack Obama, Trump amewahakikishia wafuasi wake kuwa atawatumia wahuni na wauzaji wa madawa ya kulevya wote toka Marekani.

Katika mahojiano kwenye kipindi cha CBS, 60 Minutes, Jumapili jioni, Trump amesema atajenga ukuta kutenganisha Mexico na Marekani kama alivyoahidi kwenye kampeni yake.
inadaiwa kuwa kuna zaidi ya  wahamiaji haramu takriban milioni 10 nchini Marekani.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget