http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

MABINGWA WA TANZANIA AZAM FC WAPIGWA 3 NA AL MERRICKH WAAGA MASHINDANO


MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, Azam fc  wametupwa nje ya michuano hiyo kwa wastani wa mabao 3-2.

Azam fc wamepigwa mabao 3-0 katika mechi ya marudiano iliyomalizika usiku huu mjini Khartoum, Sudan dhidi ya wenyeji Al Merrickh.
Hata hivyo wenyeji wangefunga mabao mengi zaidi kama wasingekosa penalti katika dakika ya 46′.
Mechi ya kwanza uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam, Azam walishinda mabao 2-0.
Katika mechi hiyo, Azam walipoteza nafasi nyingi za kufunga na kama wangekuwa makini wangepata ushindi mkubwa ambao ungewasaidia ugenini.
Al Merrickh walioanza fitina tangu Azam wanatua Khartoum walikuwa bora kwa kila kitu na walitumia vyema nafasi hizo tatu walizopata kati ya nyingi walizotengeneza.
Azam wameshiriki kwa mara ya kwanza ligi ya mabingwa na wametupwa nje asubuhi kabisa na sasa wanarejea kwenye mechi za ligi ambako nako kuna cheche za Yanga.
Kabla ya ligi ya mabingwa, mabingwa hao wa Tanzania waliwekeza pesa nyingi katika maandalizi, waliweka kambi uganda, wakaenda kushiriki kombe la Mapinduzi mwanzoni mwa mwaka huu na wakamalizia kambi nchini Congo DR, lakini mavuno yamekuwa hafifu.
Wakati huo huo, KMKM, wawakilishi wa Zanzibar ligi ya mabingwa wametolewa na wapinzani wakubwa wa Merrickh, Al Hilal kwa wastani wa mabao 2-0.
KMKM walishinda 1-0 jioni ya leo uwanja wa Amaan Zanzibar, lakini mechi ya kwanza walipigwa 2-0 nchini Sudan.
Tanzania imebakiwa na timu mbili tu katika mashindano ya kimataifa kwa maana ya Yanga na Polisi FC ya Zanzibar.
Yanga walifuzu raundi ya pili jana usiku kwa wastani wa mabao 3-2.
Walifungwa 2-1 na BDF XI mjini Gaborone, lakini wao walishinda 2-0 Dar es salaam.
Polisi wana uwezekano mkubwa wa kutupwa nje ya mashindano kwani mechi ya kwanza nchini Gabon, walipigwa 5-0 na CF Mounana.
Kesho wanahitaji ushindi wa magoli 6-0 ili kusonga mbele
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget