http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Washika Bunduki wa London 2-1 Crystal Palace


RAHA ipo kwa Washika Bunduki wa London, Arsenal baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.

Santi Cazorla alifungua biashara kwa kuifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya nane kwa penalti, kufuatia mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck kuangushwa kwenye boksi

Olivier Giroud akawafungia The Guuners bao la pili dakika ya 45, wakati Glenn Murray aliifungia bao la kufutia unyonge Palace dakika ya 90
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Ospina, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Sanchez/Gabriel dk89, Ozil/Rosicky dk76, Welbeck/Gibbs dk76 na Giroud.&nbsp

Crystal Palace: Speroni, Ward, Dann, Delaney, Souare, Ledley/Ameobi dk79, Zaha, Puncheon, Mutch, Gayle/Murray dk79 na Campbell/Bolasie dk57
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget