Huwezi amini: Akitokea benchi, Demba Ba aliteleza na kupiga mpira uliozama kimiani na kuiandikia Chelsea bao la pili na la ushindi.
Mwanaume: Demba Ba akishangilia bao lake lililoipeleka Chelsea nusu fainali
Maelekezo: Mourinho akiwaambia wachezaji wake walinde bao hilo la ushindi katika dakika za majeruhi
MSENEGAL `Supa Sabu` Demba Ba ameibua shangwe, nderemo na vifijo kwa mashabiki wa Chelsea waliofurika katika dimba la Stamford Bridge usiku huu baada ya kuifungia klabu yake bao muhimu katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya PSG.
Hii ilikuwa mechi ya robo fainali ya pili ambayo Chelsea walihitaji ushindi wa mabao mawili kwa bila ili kufuzu hatua ya nusu fainali kufuatia kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza nchini Ufaransa.
Chelsea wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya wastani wa magoli kuwa 3-3, lakini kwa vile wao walifunga bao moja katika kipigo cha 3-1 nchini Ufaransa wameweza kufuzu hatua ya nusu fainali.
Ba alifunga bao la pili katika dakika ya 87 na kumfanya Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ashangilie kama alivyofanya miaka ya nyuma akiwa na FC Porto.
Cesar Azpilicueta alipiga shuti ambalo liliwababatiza mabeki wa PSG na mpira kumkuta Ba akiwa eneo zuri na kumalizia kwa ufundi mkubwa mno huku mlinda mlango,Salvatore Sirigu akibaki hana la kufanya.
Wakati kila mtu akiamini Mourinho ameshatupwa nje ya mashindano, ghafla baada ya bao la nyota huyo raia wa Senegal, Jose alikimbia kutoka eneo la benchi lake kwenda kwenye kibendera cha kona kushangilia na wachezaji wake.
Mourinho amewakumbusha watu wengi miaka ya nyuma kwani aliwahi kushangilia kwa staili hiyo akiwa na FC Porto mwaka 2004 kwenye uwanja wa Old Trafford.
Hakika usiku huu ni wa furaha kubwa kwa Mourinho
kwasababu kadri muda ulivyozidi kwenda alikuwa anachanganyikiwa na kuona ndoto zake zinafifia mpaka ilipofika dakika hizo za lala salama na Ba kumnyanyua kwa shangwe.
Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na Mjerumani Andre Schurrle katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza.
Katika mechi nyingine, Real Madrid wamefuzu hatua ya nusu fainali licha ya kufungwa mabao 2-0 na Borrusia Dortmund katika dimba la Signal Iduna Park.
Madrid wamenusurika kutokana na ushindi wa mabao 3-o walioupata Santiago Bernabeu katika mchezo wa kwanza.
Real wakianza bila ya Cristiano Ronaldo ambaye hakuwa fiti kuanza mchezo wa leo, walikaribia kutolewa na
vijana wa Jurgen Klopp, lakini jitihada za mlinda mlango wao, Iker Casillas zimewaepushia balaa la kutolewa.
Hata hivyo, Real Madrid walikosa penati baada ya winga wake nyota, Angel Di Maria kuteleza wakati akipiga tuta hilo, hivyo kipa wa Borussia kuokoa kirahisi.
Hayajatosha: Marco Reus ameifungia mabao mawili Borussia Dortmund, lakini wametolewa na Real Madrid
Bahati kubwa: Kipa wa Borussia, Roman Weidenfeller akiokoa penati ya Angel Di Maria baada ya nyota huyo raia wa Argentina kuteleza wakati anapiga mpira
Haamini: Cristiano Ronaldo akiduwaa baada ya Di Maria kukosa tuta
Wamekosa bahati: Dortmund walipata nafasi nyingi za kufunga zikiwemo tatu za Henrikh Mkhitaryanwww.skychami.com
Post a Comment