http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Vidic kukosa nusufainali kutokana na kadi nyekundu aliyoonyeshwa dhidi ya chelsea


Nemanja Vidic 




Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic atakosa mechi ya nusufainali ya marudiano katika League Cup dhidi ya Sunderland uwanjani Old Trafford Jumatano baada ya kushindwa kubatilisha kadi nyekundu aliyopokezwa wikendi iliyopita.
Difenda huyo wa kati aliwasilisha malalamishi ya kutimuliwa uwanjani bila hatia baada yake kuonyeshwa kadi nyekundu wakati wa mechi ya Ligi ya Premia ambapo mabingwa United walilazwa 3-1 na Chelsea uwanjani Stamford Bridge Jumapili. Vidic alidaiwa kumchezea visivyo Eden Hazard.
Vidic alionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja, ambayo kawaida huandamana na marufuku ya kutocheza mechi tatu.

Tume huru ya kinidhamu ilithibitisha Jumanne kwamba marufuku hiyo itatekelezwa “mara moja”, kuanzia mechi ya Jumatano ambapo United wanajaribu kupindua kushindwa kwa 2-1 walikopokezwa mechi ya mkondo wa kwanza.
"Malalamishi ya Nemanja Vidic wa Manchester United kwamba alifukuzwa uwanjani kimakosa yamekataliwa na tume huru ya kinidhamu,” ilisema taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Uingereza Jumanne.
"Kwa hivyo, marufuku ya mechi tatu kwa mchezaji huyo inaanza kutekelezwa mara moja. Vidic alionyesha kadi nyekundu kwa kucheza vibaya wakati wa mechi ya timu yake dhidi ya Chelsea Jumapili 19 Januari 2014.”
Mserbia huyo wa miaka 32 pia atakosa mechi za United katika ligi dhidi ya Cardiff City nyumbani na ugenini dhidi ya Stoke City.
United walizoea kutojishughulisha sana na League Cup chini ya meneja wa zamani Alex Ferguson, ingawa walishinda kikombe hicho mara nne chini ya raia huyo wa Scotland na badala yake walisaka vikombe vya hadhi zaidi.
Lakini kufuatia kichapo cha Jumapili ambacho kimeacha timu hiyo ya David Moyes alama 14 nyuma ya viongozi wa Ligi ya Premia Arsenal, na baada ya kubanduliwa Kombe la FA na Swansea City, United wanahitaji sana ufanisi katika League Cup.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget