http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

United watwangwa mara ya tatu mfululizo mbele ya Sunderland


Sunderland walijiweka pazuri dhidi ya Manchester United kwa kushinda mechi ya kwanza ya nusufainali yao katika Kombe la Ligi 2-1 Jumanne na kumzidishia shinikizo meneja wa United David Moyes baada ya wiki ngumu.
Mwitaliano Fabio Borini alifunga penalti kipindi cha pili na kuipa timu hiyo inayoshika mkia kwenye Ligi ya Premia uongozi wa bao moja wakielekea Old Trafford kwa mechi ya marudiano.
Hii ni baada ya bao la dakika ya 52 lake Nemanja Vidic kwa kutumia kichwa kufuta bao la kujifunga la Ryan Giggs lililokuwa limeingia wavuni muda wa mwisho kipindi cha kwanza.
Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu mfululizo kwa United kushindwa baada yao kushindwa nyumbani katika Kombe la FA raundi ya tatu na Swansea City Jumapili, na pia na Tottenham Hotspur ligini wiki iliyotangulia.

Matokeo hayo yameendelea kumuongezea presha Moyes katika msimu wake wa kwanza akiwa kwenye usukani.
Mechi ya marudiano itachezwa Januari 22 kuamua nani atakutana na atakayeshinda kati ya Manchester City na West Ham United, ambao watachezea Etihad Jumatano, katika fainali Machi 2.
Kwa meneja wa United Moyes, Kombe la Capital One limeongeza umuhimu wake ikizingatiwa kwamba klabu hiyo tayari imebanduliwa kutoka kwa Kombe la FA, na pia inaonekana kutokuwa na uwezo wa kushinda Ligi ya Premia au Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kwa mashabiki ambao waliwazomea wachezaji wakiondoka uwanjani baada ya kushindwa na Swansea, hakukuwa na chochote cha kuinua nyoyo zao.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza tangu 1932 kwa United kushindwa mechi tatu za kwanza katika mwaka, na mara ya kwanza tangu 1992 kwao kushindwa mara tatu katika kipindi cha wiki moja.
Sunderland wamefika katika fainali ya Kombe la Ligi mara moja tu, mwaka 1985 ambapo walishindwa na Norwich City, na mashabiki wa klabu hiyo hawahitaji kukumbushwa kwamba walishushwa ngazi kutoka ligi kuu msimu huo.
Dimba hilo la muondoano kwa mara nyingine lilikabidhi Sunderland wakati pekee wa nafuu kwenye msimu, kwani wameshindwa mechi zote tano nyumbani katika Vikombe vya Ligi na FA.
Baada ya Giggs kugonga mwamba wa goli kwa kombora kali, mchezaji wa umri wa miaka 18 Januzaj alikuwa ametia mpira wavuni dakika saba kabla ya muda wa mapumziko lakini likakataliwa kwa kuotea.
Mwishowe, Sunderland ndio walioangukiwa na bahati dakika za mwisho za kipindi hicho. Jonny Evans aliuza frikiki na ilipotwanga na Seb Larsson mpira huo ukaingizwa wavuni na Giggs ambaye alikuwa amekabiliwa na presha kutoka kwa mchezaji wa zamani wa United Phil Bardsley.
Lilikuwa ndilo bao la kwanza kwa United kufungwa kwenye dimba hilo msimu huu.
Huzuni ya mashabiki waliokuwa wamesafiri ilipunguzwa kidogo dakika saba baada ya kipindi cha pili kuanza pale difenda wa Serbia Vidic, aliyekuwa amerejea kwenye timu hiyo, kusawazisha kwa bao la kichwa mlingoti wa mbali wa goli.
Hata hivyo, Sunderland ndio walioonyesha ukakamavu ambao umekosekana kwenye uchezaji wao ligini, na wakatwaa uongozi kupitia fowadi aliye kwao kwa mkopo kutoka kwa Liverpool Borini kupitia mkwaju wa penalti baada ya Adam Johnson kuangushwa eneo la hatari na Tom Cleverley.www.skychami.bblogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget