http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

CRISTIANO RONALDO ATIMIZA MABAO 400 KATIKA SOKA LA KULIPWA - AMFUNIKA RONALDO DE LIMA


Cristiano Ronaldo amefikisha mabao 400 tangu aanze kucheza soka la kulipwa usiku wa Jumatatu baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa ushindi wa 3-0 wa Real Madrid dhidi ya Celta katika La Liga.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya Ballon d'or wiki ijayo, alifunga jumla ya mabao 69 katika mechi 59 kwa klabu na nchi yake ndani ya mwaka 2013 na mabao yake mawili ndani ya mwaka huu 2014 yanamaanisha amefikisha jumla ya mabao 400.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mpaka sasa yupo sawa na mshambuliaji Pauleta kwa kuongoza kuifungia mabao mengi timu ya taifa ya Ureno, wote wakiwa wamefunga jumla ya mabao 47, huku akiwa amefunga mabao 353 kwenye vilabu alivyochezea, hivyo kumpita hata gwiji wa soka wa Brazil Ronaldo ambaye alifunga jumla ya mabao 352 mpaka alipostaafu soka.

Mabao 400 ya mshambuliaji huyo mzaliwa wa Madeira yamekuja baada ya michezo 653, lakini kitu cha kuvutia zaidi mreno akiwa na Real Madrid.source shaffih daudaposted by skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget