http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Navas kutochezea City nusufainali

Jesus Navas 




Winga wa Manchester City Jesus Navas atakosa mechi ya kwanza ya nusufainali Kombe la Ligi dhidi ya Westham United nyumbani Jumatano kutokana na jeraha la goti, meneja Manuel Pellegrini alifichua Jumanne.
Mhispania huyo wa umri wa miaka 28 alicheza kama nguvu mpya kipindi cha pili timu hiyo ilipotoka sare 1-1 na Blackburn Rovers katika Kombe la FA Jumamosi, lakini ingawa jeraha lake si bay asana, Pellegrini hataki kubahatisha.
“Hajajeruhiwa lakini ana tatizo ndogo,” Pellegrini alisema. “Si bay asana, ni kuchukua tu tahadhari.”
Pellegrini pia alifichua kwamba mfungaji bora wao wa mabao Sergio Aguero yuko karibu kurejea baadaye mwezi huu, baada ya kutocheza kufuatia jeraha la misuli ya chini ya mguu alilopata wakati wa ushndi wao wa 6-3 dhidi ya Arsenal Desemba 14.
"Anafanya kazi, anafanya mazoezi,” alisema raia huyo wa Chile wakati wa kikao na wanahabari cha kabla ya mechi Jumanne.

"Ni habari njema sana. Mchezaji yeyote kurudi baada ya kupona jeraha ni habari njema sana, hasa kwa mchezaji mzuri kama Kun Aguero."
Beki wa kati Martin Demichelis pia yuko sawa kucheza dhidi ya West Ham baada ya kukosa mechi nne kutokana na jeraha la misuli ya paja, lakini Micah Richards, Jack Rodwell na Stevan Jovetic hawawezi kucheza.
Pellegrini pia alisema hajaamua ni kipa yupi atachezesha kati ya Joe Hart na Costel Pantilimon.
Hart anayechezea timu ya taifa ya Uingereza alijipatia nafasi take tena kwenye timu ya kwanza majuzi baada ya kupokonywa na Pantilimon, lakini alirejea kwenye timu dhidi ya Blackburn na alifanya kosa lililopelekea wenyeji kusawazisha.
"Kesho tutaona 11 watakaoanza,” Pellegrini alisema.
"Ninafikiri (Pantilimon) amefanya vyema. Nilitathmini uchezaji wake na wachezaji na kesho tutaona ni nani ataanza.”www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget