http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Aguero akaribia kurejea Man City kuikabili Barcelona

Sergio Aguero 




Straika Sergio Aguero ameanza kufanya mazoezi na yuko karibu kurudi kuchezea Manchester City baada ya kukaa nje tangu kabla ya Krismasi kutokana na jeraha la misuli ya chini ya mguu, meneja Manuel Pellegrini alisema Jumanne.
"Ninafikiri Sergio atarejea Januari – anafanya kazi, anafanya mazoezi,” Pellegrini aliambia kikao cha wanahabari kabla ya mechi ya kwanza ya nusufainali ya leo Jumatano katika Kombe la Ligi dhidi ya West Ham.

"Bila shaka ni habari njema sana. Mchezaji yeyote kurudi baada ya kupona jeraha ni habari njema sana, hasa kwa mchezaji mzuri kama Kun Aguero."
Aguero raia wa Argentina, aliyejeruhiwa wakati wa ushindi wa 6-3 dhidi ya Arsenal, ni mmoja wa wachezaji wa City ambao hawataweza kucheza pambano hilo dhidi ya West Ham pamoja na Stevan Jovetic na Jack Rodwell huku Jesus Navas naye akiwa na “tatizo ndogo” kwenye goti lake.
"Jovetic, Aguero na Rodwell wana majeraha na kwa hivyo hawawezi kucheza kesho,” Pellegrini alisema.
"Jesus Navas ana tatizo ndogo kwenye goti lake. Si baya sana lakini tunachukua tahadhari.”
Aguero amefunga mabao 13 katika Ligi ya Premia msimu huu, ingawa kutokuwepo kwake hakujakuwa tatizo kwa City ambao wameshinda mechi tano kati ya sita katika mashindano yote tangu kuondoka kwake.
Baada ya mwanzo usio mwema kwenye ligi, hasa ugenini, City wamepata mdundo wao na Kombe la Ligi linaweza kumkabidhi Pellegrini nafasi ya mapema ya kuweka kombe lake la kwanza kwenye kabati la klabu hiyo.
Wanashikilia nambari mbili kwenye Ligi ya Premia, wana mechi ya marudiano nyumbani dhidi ya Blackburn Rovers katika Kombe la FA na wako kwenye 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
“Hatufikirii kuhusu kushinda vikombe hivyo vinne, sisi tunafikiria tu kushinda mechi inayofuata,” Pellegrini ambaye ni raia wa Chile alisema.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget