http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Mourinho asema Mikel ni 'mwenye kipaji'


John Obi Mikel 




Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho amemsifia sana kiungo wa kati wa Nigeria, John Obi Mikel.
Mourinho aliambia tovuti rasmi ya Chelsea, chelseafc.com kwamba Mikel hufanya vyema sana katika lolote analofanya.
“Mikel ana kipaji asilia katika nafasi anayocheza. Huwa ni muujiza kwake kupoteza mpira,” Mourinho alisema.
Mnigeria huyo alitua Chelsea miaka saba na nusu iliyopita akitokea klabu ya Norway, FC Lyn Oslo kama kiungo wa kati wa ulinzi.
Uchezaji wake umepigwa msasa kiasi na “Special One” (Yule wa Kipekee) lakini mchezaji huyo wa miaka 26 hawezi kulalamika kwani amefurahia maisha yake London Magharibi.
“Kuja klabu kubwa kama Chelsea, kama mchezaji chipukizi wa miaka 18 kutoka Afrika, ilikuwa ni kutimia kwa ndoto kwangu,” Mikel aliambia chelseafc.com.
Hata hivyo alifichua kwamba mambo hayakumuendea shwari siku zake za kwanza kama mchezaji wa Chelsea.

“Nakumbuka nikiingia chumba cha kubadilishia mavani na nilikuwa natetemeka wiki yote ya kwanza. Wachezaji waliokuwa huko walinisaidia sana kuzoea - John Terry, Frank Lampard, Didier Drogba na wachezaji wengine kutoka Afrika waliokuwa huko wakati huo.
“Nilikuwa nawatazama kila siku na nilijifunza mengi kutoka kwao, jinsi ya kufanya mambo uwanjani na nje, jambo lililonisaidia kukua na kukomaa kama mtu binafsi. Kilikuwa ni kipindi cha ukuaji ambacho sijawahi kuwa nacho popote. Niliingia tu moja kwa moja katika timu na nililazimika kujifunza hivyo,” akasema.
Mikel amekosolewa siku za awali kutokana na kutofunga mabao kwake lakini msimu huu amefungia Blues mawili na alisema angependa kufunga mengi zaidi.
“Bila shaka ningependa kufunga lakini si wachezaji wote 11 wanaoweza kufunga, kuna watu ambao ni wa kusimamia timu. Nikicheza na Frank huwa kila mara anaenda mbele. Sote tukienda mbele, unaweza kuwa mkasa, vile vile kwa Rami (Ramires), huwa anatoka eneo moja la hatari hadi jingine. Huwa ni lazima nihakikishe nimetulia eneo letu, na tunapokosa kufungwa na tunashinda huwa nina furaha sana,” akasema.
Mikel amechezea Chelsea mara 16 kwenye ligi msimu huu.WWW.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget