Mwenyekiti wa Eintracht Heribert Bruchhagen alithibitisha kutoka kwenye kambi ya mazoezi ya majira ya baridi ya klabu hiyo Abu Dhabi kwamba Rode, difenda mcheza kati wa umri wa miaka 23, amo njiani kujiunga na mabingwa hao wa sasa.
Rode ndiye mchezaji wa pili kuahidi kujiunga na Bayern majira ya joto yatakapofika, baada ya viongozi hao wa Bundesliga kuthibitisha kwamba wamemnasa straika wa Poland na Borussia Dortmund Robert Lewandowski baada ya kuandikiana mkataba wa mapema wikendi iliyopita.
Rode, aliyejiunga na Eintracht kutoka Kickers Offenbach mwaka 2010, alikuwa amehusishwa na kuhamia Bayern miezi kadha.
Post a Comment