http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Rooney anagonga lango la ukuu- Moyes

Wayne Rooney 
Meneja wa Manchester United, David Moyes, amesifu uwezo wa uongozi unaodhihirishwa na nyota Wayne Rooney huku akiongeza straika huyo matata anakondolea ukuu kwenye timu hiyo maarufu.
Rooney, ambaye alikuwa tashwishi kabla ya mechi ya wikendi iliyopita dhidi ya West Ham kutokana na jeraha, aliongoza wenzake kuwezeka wapinzani wao 3-1 na Moyes anaamini kuwa mshambuliaji huyo wa Uingereza amechukuwa usukani katika harakati za kuboresha wenzake.
Meneja huyo ameridhika pakubwa na tabia ya Rooney tangu achukuwe utawala wa Old Trafford huku akinogeshwa na ukomavu nyota huyo wa miaka 28 anaonyesha katika safari yake ya kutambuliwa kama mbambe wa United
.
Mshambuliaji huyo anakaribia kuathimisha mwongo mmoja kwenye timu hiyo.
“Unajua ni nini ninacho tazama zaidi ya kila kingine kwa Wayne? Naona uongozi,”Moyes alisema.
“Ninaona mtu anayetaka kutwaa jukumu la kikosi na anayejali vile yeye na wenzake wanavyocheza.”
“Pengine hajafikia kiwango chake cha ubora zaidi na wakati mwingine, nitamuhitaji kucheza kwa kina kiasi lakini hana shida yeyote na kazi anayopewa. Anafikia umri anaotambua yeye si kijana tena. Yeye ni miongoni mwa mwandamizi mmoja kikosini. Bila shaka, ananusia kutambulika miongoni mwa wakuu waliochezea timu hii.”www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget