http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Mourinho alenga kuishi Chelsea miaka 12

Jose Mourinho 
Jose Mourinho anaamini kwamba udhabiti ndio kigezo muhimu zaidi katika klabu huku akitangaza dhamira yake kusalia kwenye usukani wa Chelsea kwa miaka 12 ijayo.
Mourinho alitumikia magwiji hao wa ligi ya Premier ya Uingereza kwa misimu mitatu hapo awali kabla ya kurejea tena Stamford Bridge na ameridhika kutoka na mradi wa muda mrefu uliyoko kwenye timu hiyo.
Mwalimu huyo alizidi kudai kandarasi yake ya sasa ya miaka minne ndio ‘mbaya’ zaidi tangu kuondoka Chelsea 2007 lakini anatazamia kipindi cha mafanikio makuu na timu hiyo.

Baada ya kukamilisha safari yake na mabingwa hao wa zamani wa ligi hiyo, Mourinho anatazamia kuongoza kikosi cha taifa lake Ureno au Uingereza kucheza Dimba la Dunia.
“Natumahi baada ya miaka minne, tutaketi na kuchambua mambo yatakavyo kuwa. Tutaamua kwamba klabu nami tunafurahia kuendelea au kuagana.
“Lakini ningependa kuishi hapa kwa muda tuseme wa miaka 12. Nitakuwa na umri wa 51 mwezi ujao na baada ya miaka hiyo 12, ningelipenda kushiriki Dimba la Dunia na kikosi cha taifa haswa Ureno. Uingereza ni chaguo langu la pili,” Mourinho alisema.
“Njia bora zaidi ya usimamizi ni kuhakikisha utulivu. Ukitaka kusaidia wachezaji wanawiri, utatekeleza hayo vyema zaidi na udhabiti katika ubunifu, filosofia, muundo wa mchezo na utawala.
“Haya yote yanajili kutokana na utulizu katika ngazi za juu zaidi. Wamiliki na bodi na baada ya hapo, meneja ambaye ni wa pili kwenye orodha ya utawala.”
“Udhabiti ni muhimu. Tizama kwa mfano, Manchester United na kila mmoja anahisi kwamba David (Moyes) atapewa muda kutekeleza kazi yake kwa utulivu. Nafikiri hilo ni jambo mwafaka.”
Mourinho aliendelea kusisitiza kurejea kwake Chelsea hakukuongozwa na taki ya fedha na ingelikuwa rahisi kwake kwenda klabu kinginewww.skychami.blogspot.com.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget