http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

WENGER ‘AOTA’ FERGIE KURUDI, PELLEGRINI ADHARAU VIJEMBE VYA MOURINHO!

FERGIE_n_WENGER-KICHEKO
MOURINHO_V_REFA
PELLEGRINI: ‘SIMJUI YEYE! ALIFANYA KAZI SPAIN NA MIMI NILIKUWA KLABU NYINGINE!’
WAKATI Arsene Wenger akisema hatashangaa ikiwa Sir Alex Ferguson atarudi tena kuongoza kwenye Soka, Manuel Pellegrini amekataa kujitumbukiza kwenye kupigana vijembe na Jose Mourinho huku Timu zao, Chelsea na Manchester City, zikitarajiwa kucheza Jumapili kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
 WENGER: ‘SIR ALEX FERGUSON ANAWEZA KURUDI!’
Arsene Wenger amekiri hatastushwa ikiwa Sir Alex Fergusonatabadilika na kurudi tena kwenye Soka ndani ya Miezi 6 tangu astaafu Umeneja Manchester United.
Ingawa Sir Alex Ferguson amesisitiza hatarudi tena kufundisha Soka lakini Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal, ana wasiwasi na ametamka: “Baada Miezi 6 tutajua wazi kuhusu hili. Huwezi kuondoka moja kwa moja. Ni kama kutumia Dawa kwa Miaka 30 na ghafla kuacha!”
Maneno hayo ya Wenger yamekuja kwenye Wiki ambayo Sir Alex
Ferguson amezindua Kitabu chake, ‘Sir Alex Ferguson-My Autobiography’,  ambacho ndani yake ipo Sura nzima, iitwayo ‘Kushindana na Wenger’.
Akikiri kuwa hajasoma Kitabu hicho, Wenger amesema: “Inaelekea Ferguson alikuwa akitayarisha Kitabu chake wakati bado ni Meneja. Nadhani kila Usiku alikuwa akikaa na kuandika!”
PELLEGRINI AMDHARAU ‘MBWABWAJAJI’ MOURINHO!
Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amegomakuburuzwa na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na kuingizwa kwenye malumbano wakati Timu zao zikijitayarisha kupambana kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huko Stamford Bridge hapo Jumapili.
Pellegrini na Mourinho wanayo historia yao tangu huko Spain ambapo Mourinho alimbadili Pellegrini kuwa Meneja wa Real Madrid baada ya Pellegrini kumaliza Msimu akiwa Nafasi ya Pili nyuma ya Barcelona.
Na Mourinho amebatuka: “Nafasi ya Pili ni Timu ya Kwanza kufungwa. Kama Real wangenifukuza mimi, nisingekwenda Malaga! Ningekwenda kwenye Timu kubwa huko Italy au England!”
Lakini, licha ya kupigwa kijembe, Pellegrini amekataa kuburuzwa kwenye malumbano wakati akijitayarisha kukutana uso kwa uso na Mourinho kwa mara ya kwanza Nchini England.
Pellegrini amesema: “Huwa sijiingizi kwenye malumbano na stajiingiza sasa!”
Aliongeza: “Simjui yeye. Alifanya kazi Spain, na mimi nilikuwa Klabu nyingine. Tulicheza Real na Malaga. Hamna la zaidi, sina malalamiko na yeye!”
source soka in bongoposted by skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget