Borussia Dortmund jana iliipiga Schalke Bao 3-1 na kushinda Dabi ya Ruhr iliyochezwa Veltins Arena na Mabingwa Bayern Munich walitoka nyuma na kuichapa Hertha Berlin Bao 3-2 na kubaki kileleni mwa Bundesliga.
Dortmund walianza vizuri kwa kufunga katika Dakika ya 14 kwa Bao la Pierre-Emerick Aubameyang na Schalke, ambao Msimu uliopita waliifunga Dortmund Mechi zote mbili za Ligi, wangeweza kusawazisha lakini Penati ya Kevin
-Prince Boateng iliokolewa na Kipa Roman Weidenfeller.
Nuri Sahin akaipa Dortmund Bao la Pili katika Kipindi cha Pili na Schalke kufunga Bao lao pekee kupitia Kijana wa Miaka 18 Meyer lakini katika Dakika ya 74 Dortmund wakafunga Bao la 3 kupitia Jakub Blaszczykowski.
Bayern Munich wameendeleza wimbi lao la kutofungwa katika Mechi 35 za Bundesliga baada ya kuifunga Hertha Berlin Bao 3-2 na kubaki kileleni mwa Bundesliga.
Hertha Berlin walitangulia kufunga kupitia Adrian Ramos kutoka Colombia na Bayern wakalazimika kuwatoa Majeruhi Toni Kroos na Arjen Robben walioumia ndani ya Nusu Saa ya kwanza.
Lakini, Mario Mandzukic alieingizwa kumbadili Robben katika Dakika ya 26 aliisawazishia Bayern katika Dakika ya 29 na kufunga Bao la Pili katika Kipindi cha Pili huku Mchezaji mwingine kutoka Benchi, Mario Gotze, kupiga Bao la Tatu na kuifanyia Gemu iwe 3-1.
Anis Ben-Hatira akaipa Hertha Berlin Bao lao la Pili lakini Mechi ilimalizika Bao 3-2 kwa ushindi wa Bayern Munich.BUNDESLIGA
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Bayern Munich
|
10
|
8
|
2
|
0
|
22
|
6
|
16
|
26
|
2
|
Borussia Dortmund
|
10
|
8
|
1
|
1
|
25
|
8
|
17
|
25
|
3
|
Bayer Leverkusen
|
10
|
8
|
1
|
1
|
22
|
10
|
12
|
25
|
4
|
Hertha Berlin
|
10
|
4
|
3
|
3
|
17
|
12
|
5
|
15
|
5
|
Schalke 04
|
10
|
4
|
2
|
4
|
18
|
22
|
-4
|
14
|
Post a Comment