http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

WADAU WAISHUPALIA SERIKALI KUHUSU LESENI ZA GESI


    GesiVipiClip_3556d.jpg
Mwenyekiti wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini (CEOrt), Ali Mufuruki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
Wadau wa gesi nchini wameendelea kupinga uamuzi wa Serikali kuwaweka kando kushiriki kwenye uchimbaji wa gesi, badala yake kuwakilishwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC).
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Umoja wa Watendaji Wakuu wa Makampuni (CEOrt), Ali Mufuruki alisema hatua iliyochukuliwa na serikali itawaathiri wananchi pamoja na kampuni ya kigeni ambayo yalikuwa tayari kushirikiana na wafanyabiashara wa ndani.
"Hata wale watu wa nje ambao walikuwa wameanza kuwahusisha watu wa ndani watakuwa wameanza kujiuliza kuhusu uamuzi wao kwamba hivi tulifanya uamuzi wa busara kuwa husisha hawa, mbona viongozi wao wanasema hawafai? Hii si sawa," alisema Mafuruki na kuongeza:
"Hakuna nchi duniani ambayo imesimama na kusema kuwa watu wa ndani wasihusike kwasababu hawana uwezo, pesa na
ni mafisadi."(P.T)
Kauli ya watendaji hao inakuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi (TPSF), Dk Reginald Mengi kupinga msimamo wa serikali kuwa wafanyabiashara wa ndani hawana uwezo wa kuchimba gesi kutokana na kuwa na mitaji midogo.
Pia Mafuruki alipinga ufafanuzi uliotolewa juzi na Rais Jakaya Kikwete kuwa sekta binafsi itafuata masharti sawa na wawekezaji wa nje na kusema kuwa hatua hiyo inalenga kuwakandamiza wazawa.
"Haiwezekani sera ambayo inasimamia uendelezwaji wa hii sekta ikawa inasema kwamba wawekezaji wa nje na ndani wawe sawa, hakuna kitu kama hicho," alisema.
Alisema utafiti unaonyesha kuwa nchi za Saudi Arabia, Marekani, China, Nigeria, Malaysia na Norway zinatoa kipaumbele na ulinzi kwa wawekezaji wa ndani katika sekta ya madini na nishati kutokana na umuhimu wake katika kukuza uchumi wa nchi.
Mwenyekiti huyo alisema TPDC haina uwezo wa kushiriki uchimbaji wa gesi, ila imepewa nafasi hiyo kwa kuwa ni shirika la umma na kwamba sheria inataka iwe hivyo.
"Kwa nini Serikali ibague, au kwasababu TPDC ni shirika la umma? Sawa wao washiriki lakini na sekta binafsi waruhusiwe... kutumia kampuni moja ni kujiweka kwenye hatari, kwa sababu linaweza kufa na hakuna ambaye anaweza kuniambia haiwezi kufa," aliongeza.
Alipendekeza kuwepo kwa sheria za upendeleo kwa wazawa katika sekta mbalimbali ili kuwanufaisha wadau wengi zaidi.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt, Santina Benson alisema lazima serikali ijifunze kutokana na makosa kwa kuangalia sera ya madini ambayo imeshindwa kuwanufaisha Watanzania wote

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget