http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

HAKUNA ASIYEJUA 'KUKUNJA CHAPAT'I KWA HERI RAISI TENGA TFF.

nysamlani_07757.jpg
Athumani Nyamlani
malinzi_0da5c.jpg
Jamal Malinzi

LEO hii ulimwengu wa soka unasikilizia matokeo ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho la (MNYAMA).
Kandanda Tanzania (TFF)unaofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Kufanyika kwa uchaguzi huu ni mafanikio mengine ya kuondoa sintofahamu iliyokuwepo baada ya kuahirishwa mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo za wagombea kukata rufaa FIFA kupinga kuenguliwa.
Lakini sasa mambo yote yako sawa na jana TFF ilifanya Mkutano wake Mkuu kabla ya kuelekea uchaguzi huu wa
leo.
Rais anayemaliza muda wake, Leodegar Chillah Tenga, ameendelea kuiweka rekodi yake safi katika soka la Tanzania tangu alipokuwa anacheza soka na hata kuiongoza Taifa Stars kwenye Kombe la Mataifa Afrika kule Lagos, Nigeria mwaka 1980.
Tumeona mafanikio mengi katika miaka nane aliyokuwepo madarakani, ingawa wapo watu ambao wanaendelea kubeza. Duniani hakuna anayeweza kuridhika kwa asilimia 100, hivyo ni mambo ya kawaida kabisa haya.
Soka lililokosa mwelekeo wakati wa iliyokuwa FAT lilibadilika ghafla tangu mwaka 2004 TFF ilipoundwa na uongozi mpya kushika madaraka.
Kitu pekee ambacho kimeonekana kuwa dhahiri ni kwamba, uongozi wa soka sasa unashikiliwa na wanaoujua mchezo wenyewe, tofauti na miaka ile ambapo yeyote mwenye ushawishi – wa fedha na maneno – aliweza kuongoza hata kama haweza kupiga danadana mpira.
Wagombe wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa leo ni Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emily Malinzi (Rais), Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6- Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na Mbeya).
James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam).

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget