http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

BARCELONA YATAMBA EL CLASICO YAICHAPA REAL 2-1

EL_CLASICO-BEST
NOU CAMP ilikuwa ni furaha tupu baada ya FC Barcelona kuwachapa Wapinzani wao wakubwa huko Spain, Real Madrid, Bao 2-1 katika Mechi ya La Liga ambayo imewafanya wabakie kileleni.
Kipigo hiki kimewabakiza Real Madrid Nafasi ya 3 sasa wakiwa Pointi 6 nyuma ya Barcelona.

 Barca ndio walianza kufunga kwa Bao la Kijana wao mpya kutoka Brazil, Neymar, ambae baada ya kupata pasi kutoka kwa Andres Iniesta alipiga hatua kadhaa na kuachia kiki ya chini iliyomparaza Beki wa Real Pepe na kumhadaa Kipa Diego Lopez.
Katika Dakika ya 78, Alexis Sanchez aliifungia Barca Bao zuri baada kupiga Mpira wa juu uliomzidi kimo Kipa Lopez na kutikisa nyavu.
Real walipata Bao lao moja katika Dakika za nyongeza mfungaji akiwa Jese Rodriguez alietokea Benchi alipopiga kiki ya chinichini baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Cristiano Ronaldo.
Hakika Mechi hii ilikuwa ni burudani nzuri kwa Wapenda Soka.
VIKOSI:
Real Madrid: Lopez, Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo; Pepe, Khedira; Bale, Modric, Di Maria, Ronaldo.
Akiba: Casillas, Coentrao, Benzema, Arbeloa, Jese, Isco, Illarramendi.
Barcelona: Valdes, Alves, Pique, Mascherano, Adriano; Busquets, Xavi, Iniesta; Messi, Fabregas, Neymar.
Akiba: Pinto, Montoya, Song, Puyol, Sergi Roberto, Pedro, Alexis.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget