Vichwa vya Kipindi cha Pili vya Wayne Rooney na Javier Hernandez ‘Chicharito’ vimewapa ushindi Manchester United wa Bao 3-2 dhidi ya Stoke City Uwanjani Old Trafford baada ya mara mbili kutoka nyuma.
Hadi Mapumziko, Man United walikuwa nyuma kwa Bao 2-1 kwa Bao za Peter Crouch na Marko Arnautovic huku Bao lao moja la Man United likifungwa na Robin van Persie.
Zikiwa zimebaki Dakika 12, Bao za Wayne Rooney na Chicharito, alieingia kutoka Benchi, ndizo ziliwakomboa Mabingwa hao na kuwapa ushindi wa Bao 3-2.
ASTON VILLA 0 EVERTON 0
Romelu Lukaku aliifungia Everton Bao lake la 5 katika Mechi 5 wakati walipoibwaga Aston Villa iliyokuwa Uwanjani kwao Villa Park Bao 2-0 huku Bao jingine la Everton likifungwa na Leon Osman
Awali Christian Benteke wa Villa alikosa kufunga kwa Penati ambayo iliokolewa na Kipa Tim Howard.
Huu ni ushindi wa 5 kwa Everton katika Mechi zao 6 za Ligi walizocheza mwisho.
LIVERPOOL 4 WEST BROM 1
Luis Suarez leo Uwanjani Anfield alipiga Hetitriki na Daniel Sturridge kufunga Bao moja wakati Liverpool ilipoichapa West Brom Bao 4-1.
Bao la West Brom lilifungwa na James Morrison kwa Penati.
NORWICH CITY 0 CARDIFF CITY 0
Kipa wa Cardiff City, David Marshall, leo alikuwa shujaa baada ya kuizuia Norwich City kupata Bao Uwanjani kwao Carrow Road katika Mechi ambayo ni mara ya kwanza kwa Timu hizi kukutana katika Ligi Kuu England.
CRYSTAL PALACE 0 ARSENAL 2
Arsenal wameichapa Timu isiyokuwa na Meneja Crystal Palace Bao 2-0 na kubakia kileleni mwa Ligi licha ya kucheza Mtu 10 baada ya Kiungo wao Mikel Arteta kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Arteta ndie alieifungia Arsenal Bao la kwanza kwa Penati ya Dakika ya 47 iliyotolewa baada ya Adlene Guedioura kumchezea rafu Serge Gnabry.
Katika Dakika ya 65, Arteta alipewa Kadi Nyekundu baada kumchezea rafu Marouane Chamakh aliekuwa akichanja mbuga na Refa kumtoa kwa vile yeye alikuwa ndie Mtu wa mwisho kwenye Difensi.
Olivier Giroud aliifungia Arsenal Bao la Pili katika Dakika ya 87.
KUANZIA JUMAPILI, MAJIRA HUKO ENGLAND YANABADILIKA.
MECHI ZITAANZA KUCHEZWA SAA 1 MBELE YA TILIVYOZOEA BONGO
TOFAUTI YA MASAA ITAKUWA NI MATATU [BONGO WATAKUWA SAA 3 MBELE]
Post a Comment