http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

WIMBI LA MADAWA YA KULEVYA LAENDELEA KUSHAMIRI



Mnigeria akamatwa Kenya na dawa za kulevya, inaaminika alipitia airport ya Julius Nyerere

442203-heroinRaia wa Nigeria aliyefukuzwa nchini Kenya kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya amekamatwa jijini Nairobi na inaaminika amepitia kwenye airport ya Julius Nyerere na kupitia mpaka wa Namanga. Enobemhe Emanuel Peter amekamatwa na pakiti 425 za Heroin huko jijini Nairobi. Mnigeria huyu ni moja kati ya watu waliofukuzwa nchini Kenya kwa agizo la Rais Uhuru Kenyatta kuwafukuza watu wote wanaojihusisha na biashara za dawa ya kulevya.
Idara ya uhamiaji Tanzania wamesema “Mtu akifukuzwa na nchi moja haimaanishi kwamba haruhusiwi kuingia nchi nyingine. Kama jirani zetu wangekuwa na ushirikiano na sisi baada ya kumkata mtu,wangetupa taarifa ili anapoingia Tanzania tunakuwa makini naye. Huyo mtu alipita tu hapa Tanzania”.  So, haijulikani kama mtu huyo alipita airport ya Julius Nyerere na hizo dawa au la.
Imeripotiwa na gazeti la Mwananchi Sept 16.


Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget