http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

EFA CHAMPIONZ LIGI: MECHI MAKUNDI KUANZA KESHO JUMANNE!

UCL_2013_LOGO
UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, inaanza hatua yake ya Makundi kesho Jumanne Septemba 17 na Jumatano Septemba 18 huku Mabingwa Watetezi Bayern Munich wakianza Nyumbani kucheza na CSKA Moscow na zifuatazo ni Dondoo muhimu za Timu zote kwenye Mechi hizo za kwanza.
 
RATIBA:
[Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu]
Jumanne 17 Sep 2013
Manchester United FC v Bayer 04 Leverkusen
Real Sociedad de Fútbol v FC Shakhtar Donetsk
Galatasaray A.Ş. v Real Madrid CF
FC København v Juventus
SL Benfica v RSC Anderlecht
Olympiacos FC v Paris Saint-Germain
FC Bayern München v PFC CSKA Moscow
FC Viktoria Plzeň v Manchester City FC
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 04 v FC Steaua Bucureşti
Chelsea FC v FC Basel 1893
Olympique de Marseille v Arsenal FC
SSC Napoli v Borussia Dortmund
FK Austria Wien v FC Porto
Club Atlético de Madrid v Football Club Zenit
AC Milan v Celtic FC
FC Barcelona v AFC Ajax

MECHI ZA JUMANNE SEPTEMBA 17
KUNDI A
-Manchester United FC v Bayer 04 Leverkusen
-Real Sociedad de Fútbol v FC Shakhtar Donetsk
• Hii ni mara ya 18 mfululizo kwa Man United kushiriki kampeni za UCL lakini kwa Meneja wao mpya, David Moyes, hii ni mara ya kwanza kwake kucheza Hatua ya Makundi ya Mashindano haya ambayo Klabu yake imeyatwaa mara 3. Vile vile, Kwa Meneja wa Bayer Leverkusen, Sami Hyypia, hii ni mara ya kwanza kuongoza Timu kwenye UCL lakini ameshawahi kutwaa Ubingwa akiwa Mchezaji wa Liverpool Mwaka 2005.
• Shakhtar Donetsk wanashiriki Makundi ya UCL kwa mara yao ya 9 lakini Real Sociedad hii ni mara yao ya kwanza tangu wacheze hatua hii Msimu wa 2003/04. KUNDI B
-Galatasaray AŞ v Real Madrid CF
-FC København v Juventus
• Kocha wa Galatasaray Fatih Terim alikuwa AC Milan Msimu wa 2001/02 na kubadilishwa na Carlo Ancelotti. Ümit Davala, ambae sasa ni Kocha Msaidizi Galatasaray, alicheza Mechi 7 Msimu huo huo chini ya Ancelotti.
• Hii ni mara ya pili kwa Miaka miwili mfululizo kwa Juve kwenda kucheza Copenhagen na Msimu uliopita kwenye Makundi ya UCL walitoka Sare 1-1 na FC Nordsjælland kwa Bao la Dakika ya mwisho la Mirko Vučinić.
KUNDI C
-SL Benfica v RSC Anderlecht
-Olympiacos FC v Paris Saint-Germain FC)
• Mwaka 1983 katika Fainali ya UEFA Cup, Anderlecht waliifunga Benfica Bao 1-0 Nyumbani na kutoka Sare 1-1 huko Lisbon na kunyakua Kombe. Kocha Msaidizi wa sasa wa Benfica, Minervino Pietra, na Katibu wa Ufundi wa Klabu hiyo, Shéu Han, wote walicheza Fainali hiyo.
• Kocha wa PSG Laurent Blanc na Kocha wa Olympiacos Míchel walikutana uso kwa uso wakati France na Spain zilipocheza Mechi ya Mchujo ya EURO 1992 Mjini Paris hapo Tarehe 20 Februari 1991 na Blanc alifunga Bao la mwisho la France waliposhinda 3-1.
KUNDI D
-FC Bayern München v PFC CSKA Moscow
-FC Viktoria Plzeň v Manchester City FC
• Kocha wa Bayern Josep Guardiola alikuwemo kwenye Timu ya FC Barcelona, ambayo wakiwa Mabingwa Watetezi, walitolewa kwenye Raundi ya Pili na CSKA Moscow katika Msimu wa UCL wa 1992/93 UEFA Champions League walipofungwa Nyumbani 3-2 na CSKA kufuatia Sare ya 1-1 katika Mechi ya Kwanza.
• Wakati Man City wameingia moja kwa moja Hatua hii ya Makundi baada ya kumaliza Washindi wa Pili wa Ligi Kuu England, Viktoria Plzeň, ambao ni Mabingwa wa Czech Republic, imebidi washinde Raundi za Mchujo tatu za awali za Mashindano haya kwa kushinda Mechi zao zote 6  Plzeň kwa kuzifunga FK Željezničar Jumla ya Mabao 6-4 kwa Mechi mbili, JK Nõmme Kalju Jumla 10-2 na NK Maribor Jumla 4-1.
MECHI ZA JUMANNE SEPTEMBA 18
KUNDI E
-FC Schalke 04 v FC Steaua Bucureşti
-Chelsea FC v FC Basel 1893
• Steaua Bucharest hawajawahi kuifunga Klabu yeyote ya Germany kwenye Mechi zinazochezwa Nchini humo na wamefungwa Mechi 6 na Sare 3.
• Chelsea na Basel zilikutana Msimu uliopita kwenye Nusu Fainali ya UEFA Europa LIGI na Chelsea kushinda kwa Jumla ya Mabao 5-2 na kutua Fainali waliyotwaa Kombe hilo.
KUNDI F
-Olympique de Marseille v Arsenal FC
SSC Napoli v Borussia Dortmund
• Misimu miwili iliyopita, OM na Arsenal walikuwa Kundi moja kwenye UCL na wao kunyakua Nafasi mbili za juu na kusonga mbele. Katika Mechi zao, Arsenal walishinda 1-0 kwa Goli la Dakika za mwisho la Aaron Ramsey na kwenye Marudio kutoka 0-0.
• Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Napoli na Dortmund kukutana katika Mashindano rasmi lakini Napoli wana Rekodi mbovu mno dhidi ya Klabu za Germany ambazo katika Mechi zao 7 za mwisho hawajashinda hata Mechi moja na kufungwa Mechi 5.
KUNDI G
-FK Austria Wien v FC Porto
-Club Atlético de Madrid v FC Zenit
• Porto wanatua kwenye Uwanja ambao uliwapa Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza Mwaka 1987 walipoifunga Bayern Munich Bao 2-1.
• Mwaka mmoja uliopita, Zenit walisafiri kwenda Madrid na kufungwa 3-0 na Málaga CF kwenye Hatua ya Makundi ya UCL. Msimu uliopita, Atlético walitolewa kwenye UEFA Europa LIGI na Klabu ya Russia FC Rubin Kazan.
KUNDI H
-AC Milan v Celtic FC
FC Barcelona v AFC Ajax
• Mchezaji mpya wa AC Milan, Alessandro Matri, Msimu uliopita alifunga Bao katika kila Mechi walipoifunga Celtic Jumla ya Mabao 5-0 kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL wakati akiichezea Juventus.
• Ajabu ni kwamba hii ni Mechi ya kwanza kabisa kati ya Barcelona na Ajax kwenye Mashindano ya Ulaya.
MECHI ZIFUATAZO:
Jumanne 1 Oktoba 2013
FC Basel 1893 v FC Schalke 04
FC Steaua Bucureşti v Chelsea FC
Borussia Dortmund v Olympique de Marseille
Arsenal FC v SSC Napoli
Football Club Zenit v FK Austria Wien
FC Porto Club v Atlético de Madrid
AFC Ajax v AC Milan
Celtic FC v FC Barcelona
Jumatano 2 Oktoba 2013
FC Shakhtar Donetsk v Manchester United FC
Bayer 04 Leverkusen v Real Sociedad de Fútbol
Juventus v Galatasaray A.Ş.
Real Madrid CF FC København
Paris Saint-Germain v SL Benfica
RSC Anderlecht v Olympiacos FC
Manchester City FC v FC Bayern München
PFC CSKA Moskva v FC Viktoria Plzeň

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget