http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

AGUERO NA WENZAKE WAWEZEKA JUU YA CHELSEA NA MAN U.

AGUERO NA WENZAKE WAZIOGOPA MAN UNITED & CHELSEA!

SERGIO_AGUEROSTRAIKA wa Manchester City Sergio Aguero amekiri kuwa yeye na Wachezaji wenzake wana wasiwasi na Mabingwa Manchester United na Chelsea kuwa ndio changamoto kwao kuweza kutwaa Ubingwa Msimu huu.
Aguero, Miaka 25, ambae ndie aliefunga Bao Sekunde za mwisho na kuipa Man City Ubingwa wao wa kwanza katika Miaka 44 Mwezi Mei Mwaka 2012 walipoifunga QPR Bao 3-2, pia amesema yeye binafsi anawania kupata Buti ya Dhahabu Msimu huu.
Lakini licha ya kuzigwaya Man United na Chelsea, Aguero, ambae sasa yuko na Kikosi cha Argentina kwa ajili ya Mechi za Kombe la Dunia, amesema wao wana imani na Kocha wao mpya kutoka Chile, Manuel Pellegrini.
Aguero alisema: “Man United watapigana chini ya Meneja wao mpya kubaki na Ubingwa wao na pia wana Kikosi kikali! Chelsea ni hatari na chini ya Jose Mourinho ni wazi watakuwa bora! Lakini na sisi tuna Meneja mpya na Timu nyingine zinatukodolea macho wakijua tunaweza kutwaa Ubingwa! ”
Hata hivyo, Man City wameanza kwa kusuasua katika Ligi Kuu England Msimu huu mpya kwani baada ya kuifunga Newcastle wakapigwa na Cardiff City katika Mechi yao ya pili na kisha kuhenyeshwa katika ushindi wao na Hull City.
Lakini hayo hayakumteteresha Aguero ambae amesema: “Kila Meneja ni tofauti lakini Kikosi kizima kinajisikia raha na Mazoezi yake na amezungumza na kila Mchezaji. Hata Wachezaji wapya wamejumuika vizuri. Nategemea kufunga Goli nyingi na kusaidia kutwaa Ubingwa. Ni wazi kazi yangu ni kufunga na kutengeneza Magoli lakini Matokeo ya Timu ndio muhimu zaidi na nitafurahi tukiwa tunashinda!”

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget