http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

WAGOMBEA TFF, TPL BOARD WAWEKEWA PINGAMIZI!

KAMATI ya Uchaguzi ya TFF leo limesambaza Taarifa iliyosainiwa na Katibu wake Angetile Osiah kuhusu kuwekewa kwa pingamizi kwa Wagombea Uongozi wa TFF na Tanzania Premier Board, TPL Board.
Kwa Wagombea nafasi ya Urais TFF waliowekewa pingamizi ni Athumani J Nyamlani ambae amewekewa pingamizi na Mintanga Yusuph Gacha na Medard Justiniani huku Mgombea mwingine wa Urais, Jamal Malinzi, akipingwa na Agapo Guo.
Michael Wambura anaeomba nafasi ya Makamu wa Rais Tff amepingwa na Josea Samuel Msengi na Said Rubea Tamim.
Wagombea wengine waliowekewa pingamizi ni wale wa nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji TFF ambao ni Epaphra Swai, Eliud P. Mvella na Athumani K. Kambi.
Kwenye TPL Board pingamizi lipo kwa Wagomgea nafasi ya Mwenyekiti ambao ni Hamad Yahya Juma aliwekewa pingamizi na Frank M. Mchaki na Yusuf Manji aliwekewa pingamizi na Daniel T. Kamna na Juma Ally Magoma.
TFF_LOGO12Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa TPL Board, Said Mohamed, yeye amewekewa pingamizi na Frank M. Mchaki.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF itakaa Jumatano Januari 30 kupitia pingamizi hizo.
Release No. 014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 27, 2013
PAMBANO LA LYON, SIMBA LAINGIZA MIL 53/-
Mechi namba 92 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Januari 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 limeingiza sh. 53,756,000.
Watazamaji 9,408 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 12,499,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,200,067.80.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 6,355,806.33, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 3,813,483.80, Kamati ya Ligi sh. 3,813,483.80, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,906,741.90 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,483,021.48.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget