Shirikisho la soka barani Africa (Confederation of African Football) lipo mbioni kufanya uchunguzi kufatia madai ya Congo fanya udanganyifu kwa kumchezesha mchezaji anayedhaniwa kuvuka umri kwenye mechi za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wa U17.
Congo-Brazzaville imefanikiwa kufuzu fainali hizo zitakazofanya mwaka ujao huko Madagascar baada ya kuiondosha Tanzania raundi ya mwisho ya kuwania kufuzu.
Laikini Tanzania ilipeleka malalamiko yake ikidai wapinzani wao kutumia wachezaji waliovuka umri uliowekwa na Caf kwenye mashindano husuka.
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) liliindikia Caf likitaka wachezaji wanaolalamikiwa kuvuka umri wafanyiwe vipimo vya kuhakiki umri wao.
Kwa upande wao Caf wamemtaja mchezaji mmoja Langa-Lesse Bercy kwa ajili ya kumfanyia vipimo kwasababu Namibia (litolewa na Congo) waliwahi kulalamikia umri wa mchezaji huyo.
Mkurugenzi wa tiba wa Caf Dr Boubakary Sidiki amethibitisha kwa kuiandikia barua TFF kwamba, Bercy ambaye alifunga magoli dhidi ya Namibia na Tanzania na kuisaidia nchi yake kufuzu, atafanyiwa vipimo November 18 jijini Cairo, Misri.
Bercy atasafiri hadi Misri aiambatana na daktari wake wakati TFF pia watatuma madaktari wao kwa ajili ya kushuhudia zoezi hilo la upimwaji wa mchezaji anayelalamikiwa.
TFF pia watalipia gharama zote zitakazohitajikana Caf.
Kwa mujibu wa kanuni za Caf, udanganyifu wa umri ni kosa ambalo linapelekea nchi husika kufungiwa miaka mitatu kushiriki mashindano ya umri husika.
Nchi nne zitakazofanikiwa kucheza nusu fainali ya mashindano hayo, zitakuwa zimefuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia chini ya miaka 17 zitakazofanyika India.
Post a Comment