http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Pedro Rodriguez kujiunga na chelsea baada ya kukosa raha pale Barcelona


Mwanzoni kabisa wa kipindi cha usajili Jose Mourinho alisema kwamba kwenye kipindi hiki cha usajili hatafanya sana usajili kwasababu anakikosi kizuri.
Lakini pia alisema atafanya usajili mdogo tu kuziba sehemu ambazo anadhani zinahitaji usajili.
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amepanga kuwania saini ya mshambuliaji Mhispania, Pedro Rodriguez anayekipiga Fc Barcelona kwa ada ya pauni milioni 22.
Pedro ambaye hafurahii maisha hivi sasa kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Ulaya. Mfumo wa sasa wa 4; 3; 3 unamnyima nafasi Pedro kutokana na uwepo wa Messi, Suarez na Neymar.
Gazeti la Sports la nchini Uhispania linaripoti kuwa kijana huyo hatakiwi katika kikosi hicho na hivyo anaweza kuondoka katika majira haya ya joto.

Inaelezwa kuwa Barcelona wako tayari kumuachia mshambuliaji huyo kwa ada ya pauni 22m.
Pedro ambaye hapati nafasi hivi sasa katika kikosi cha Barcelona anaamini anaweza kupata dakika nyingi za kucheza tofauti na ilivyo sasa Camp Nou.
Kuelewana kwa ushirikiano wa washambuliaji watatu wa kiwango cha dunia, Messi, Suarez na Neymah unamfanya kocha wa Barcelona, Luiz Enrique kutomuangalia Pedro.
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget