DUNIA haikaukiwi matukio ya
kustaajabisha, kwa hakika huu ni ulimwengu maridhawa na hawakukosea walionena
kwamba dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Stori ya kusikitisha, inatokea
nchini Marekani ambako kijana Justin Street, amepoteza maisha akiwa kwenye
jaribio la kuongeza ukubwa wa nyeti yake.
Habari kamili ipo hivi; Justin,
22, akiwa baba wa watoto wawili alikwenda kwa mwanamama Kasia Rivera ,35, aliyejitangaza
kuwa ni mtaalamu wa tiba za kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume.
Kasia aliweka matangazo
barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume, hivyo kumfanya
Justin ahamasike kwenda kupata dawa hiyo ili kujiongezea ushababi.
Wanasema tamaa mbele mauti
nyuma, ndivyo ilivyotokea kwa Justin, kwani baada ya kuomba dawa ya kuongeza
ukubwa wa maumbile yake ya kiume, alidungwa sindano yenye madini ya silikoni.
Madini hayo, alidungwa kwenye
nyeti yenyewe na baada ya muda mfupi, hali ya afya yake ilibadilika kuwa mbaya,
alizorota na siku iliyofuata alifariki dunia.
Kutokana na tatizo hilo, Kasia
alifikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji akituhumiwa kufungua zahanati bubu
ndani ya nyumba yake iliyopo New Jersey, vilevile kutoa tiba za kiafya wakati
hana taaluma hiyo wala leseni ya kuendesha kazi hiyo ya utoaji huduma za afya.
Kasia alipandishwa kizimbani
wiki iliyopita, uchunguzi wa maiti umethibitisha kwamba Justin alifikwa na
mauti baada ya madini ya silikoni aliyodungwa kwa sindano kuziba njia za
mishipa ya damu.
Mmoja wa madaktari waliomfanyia
uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kusikia silikoni
inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya wanawake imetumika kwenye kuongeza
ukubwa wa uume.Kasia, amekana kuhusika na mauaji.
Post a Comment