Uwanja wa Etihad Jijini Manchester utalipuka
kwa mpambano mkali wa Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI kati ya Manchester City na FC Barcelona.
Mechi
hii ni Marudio ya Mechi ya Msimu uliopita ya Raundi hii hii ya Mashindano haya
wakati Man City ilipotolewa na Barcelona kwa Jumla ya Mabao 4-1 katika Mechi
mbili ambazo kila Mechi City ilimaliza Mtu 10 baada ya Mchezaji wao mmoja
kupewa Kadi Nyekundu.
Katika
Mechi hizo, Barcelona walishinda Mechi ya Kwanza iliyochezwa Etihad Bao 2-0 na
kwenye
Marudiano huko Nou Camp, Barca ilishinda Bao 2-1.
Hali
za Timu
Man
City itamkosa Kiungo wao mahiri Yaya Toure ambae anamalizia Kifungo chake cha
Mechi 3 alichopewa na UEFA lakini Straika wao mpya Wilfried Bony ruksa kuanza
Mechi hii.
Barcelona
huenda wakamchezesha Straika wao Luis Suarez ambae atakuwa akicheza Mechi yake
ya kwanza Nchini England tangu aihame Liverpool mwanzoni mwa Msimu.
Tathmini
Man
City walishindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI katika Misimu
ya 2011/12 na 2012/13 lakini katika Misimu miwli iliyopita walivuka na kukwamia
hatua ya Raundi hii.
Wikiendi
iliyopita, Timu zote zilikuwa kwenye Ligi za kwao kwa Barcelona kuchapwa kwao
Nou Camp Bao 1-0 na Malaga katika La Liga baada ya kushinda Mechi 11 mfululizo
wakati City ikiitwanga Newcastle United Bao 5-0 kwenye Ligi Kuu England.
Timu
zote hizo mbili zinashika Nafasi za Pili za Ligi za Nchi zao.
Akiongelea
mtanange huu wa Uwanja wa Etihad, Sentahafu wa Barca, Gerard Pique, ambae
aliichezea Man United ambao ni Mahasimu wakuwa wa City, alisema: “Hii ni moja
ya Gemu ya Mwaka, na ni muhimu kwetu kwa sasa. Watajaribu kutushambulia na hilo
linatufaa sisi. Imedhihirishwa kwamba tunakuwa vyema dhidi ya Timu
zinazotushambulia kwa sababu tunaweza kupiga kaunta ataki!”
Nae
Straika wa Man City, Sergio Aguero, ametamka: “Hii ni Gemu mpya na sisi sasa si
sawa na Msimu uliopita na wao pia sivyo!”
Meneja
wa City Manuel Pellegrini ameahidi Timu yake itacheza kwa kushambulia tu.
Post a Comment