http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Robert Lewandowski kujiunga na Bayern msimu ujao

Robert Lewandowski 

straika wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski atajiunga na wapinzani Bayern Munich kama alivyotarajiwa majira ya joto baada ya kutia saini mkataba wa miaka mitano, mabingwa hao wa Bundesliga walithibitisha Jumamosi.
Mkataba wa Lewandowski na Dortmund unafikia kikomo mwisho wa msimu na mchezaji huyo wa umri wa miaka 25 alikuwa huru kutia saini mkataba wa mapema tangu Januari 1.
Mkataba huo wa kuhama, ambao utaanza kutumika kuanzia Julai 1, uliafikiwa baada ya Lewandowski kupita uchunguzi wa kimatibabu aliofanyiwa na daktari wa klabu Hans-Wilhelm Mueller-Wohlfahrt mjini Munich awali Jumamosi
.
"Tuna furaha kwamba tumefanikiwa katika kuhama kwa mchezaji huyu,” alisema mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge. "Robert Lewandowski ni mmoja wa mastraika bora zaidi duniani. Ataimarisha kikosi cha Bayern na kutuwezesha kupambana hata zaidi. Tuna furaha kwamba mkataba wa miaka mitano hadi 2019 umetiwa saini na pande zote mbili.”
Lewandowski alijiunga na Dortmund akitokea Lech Poznan kwa €4.5 milioni 2010 na alikuwa karibu kuhamia Bayern kipindi cha majira ya joto kilichopita. Hata hivyo, mkataba wake ulitibuka pale Dortmund walipodai ada ya kuhama inayokisiwa kuwa €25 milioni ingawa alikuwa na mwaka mmoja pekee uliokuwa umesalia kwenye mkataba wake.
Straika huyo kwa sasa anashikilia nafasi ya ufungaji bora wa mabao Bundesliga pamoja na Adrian Ramos wa Hertha Berlin na mabao 11 na kwa jumla katika Bundesliga amefunga magoli 65 baada ya kucheza mechi 115www.skychami.blogspot.com.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget