http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Mourinho akanusha kuwepo walaghai Chelsea

Jose Mourinho 
Chelsea si timu ya wachezaji wa kujiangusha kulingana na meneja wao, Jose Mourinho, baada ya mchezaji wa pili kuonywa dhidi ya tabia hiyo Jumapili.
Kiungo Ramires alipewa kadi ya njano na refarii Andre Marriner kwa kulaghai pale alipojiangusha katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Derby County.
Mwenzake kutoka Brazil, Oscar, alipokea adhabu sawia kutoka muamuzi Martin Atkinson kwenye mechi ya Ligi ya Premier Jumatano iliopita.

Hayo yalijili baada ya Mourinho kukashifu vikali nyota wa Liverpool, Luis Suarez, akidai kuwa alijiangusha kwenye ushindi wao wa 2-1 Desemba 26.
“Ninashikilia dhati kwamba hakuna walaghai. Hivi ni visa vya kipekee na ninaunga mkono marefa, wacha tuone kama vilabu vingine vitafanya hivyo.
“Nilifurahia kadi hiyo, Artkinson alifanya vyema. Wakati huu, sikuzungumuza na Ramires lakini ikiwa refa alishuhudia na atatoa uamuzi mwema, hilo ni safi kabisa,” Mourinho alisema.
Chelsea walifuzu raundi ya nne ya Kombe la FA na watakaribisha Stoke City baada ya John Obi Mikel na                                                                                  Oscar kuwafungia mabao ya ushindi.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget