http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Kagawa aahidi kufannya vizuri


Shinji Kagawa 





Kiungo wa Manchester United, Shinji Kagawa, amekiri anastahili kushamiri ikiwa huduma zake zitahitajika kila mara Old Trafford.
Mchezaji huyo nyota wa zamani wa Borussia Dortmund amekumbwa na tatizo la kujikita kwenye kikosi kikuu cha United tangu akamilishe uhamisho wa Pauni milioni 12 za Uingereza mwakani 2012.
Kufikia sasa, ameanza mechi 24 za ligi ya Premier lakini alisifiwa kwa mchezo wake wembe kwenye kipindi cha pili cha mechi yao dhidi ya Swansea wikendi iliyopita akitumika katika kitengo anachopendelea cha kiungo wa kati.
“Naweza ongeza hima kwani miye si mchezaji mrefu au mkubwa zaidi kwa hivyo, nilazima nisongeshe mwili wangu zaidi.
“Wachezaji wadogo ligi ya Premier ni wastadi wa kutumia miili yao na hilo ndilo nitaendelea kufanya kwani shindano hili ni ligumu,” Kagawa aliambia tovuti ya United.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget