http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Chelsea kukutana na man City raundi ya tano, Arsenal dhidi ya Liverpool


Laurent Kolscieny 



Chelsea watamenyana na Manchester City huku Arsenal wakitoana jasho na Liverpool kufuatia droo ya michuano ya kombe la FA ya mchujo wa raundi ya tano.
Chelsea wamefuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa 1-0.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii amesema, "Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora."
Nao Manchester City walijikatia tiketi ya kufuzu kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.
Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mechi ingine kali.
Roberto Martinez ataiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani Swansea, ilihali Sunderland watacheza na Southampton ikiwa ni mechi liyokutanisha timu zote za ligi ya Premier.
Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na Brighton. Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.
Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.
Mshindi wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainal yake itachezwa kwenye uwanja wa Wembley.
Droo kamili

Manchester City v Chelsea
Sheffield United au Fulham v Nottingham Forest au Preston North End
Arsenal v Liverpool
Brighton & Hove Albion v Hull City
Cardiff City v Wigan Athletic
Sheffield Wednesday v Charlton Athletic
Sunderland v Southampton
Everton v Swansea Citywww.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget