http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Buriani Ariel Sharon


 Ibaada maalum ya aliyekuwa waziri mkuunchini Israel Ariel Sharon imefanyika nje ya majengo ya bunge la Israel.

 Wageni waliofika kwa ibada maalum ya Sharon walimsifu kama kiongozi aliyepigania waisraeli                                                                                 

Bwana Sharon atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa taifa la Israel lakini pia alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa jasiri aliyechukiwa na wapalestina wengi.


Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alisema kuwa Sharon alikuwa mmoja wa makamanda wakuu wa wayahudi na ambaye atakumbukwa zaidi ya wote.Waliohutubia umati,wamemtaja Sharon kama mtu aliyejitolea kuhakikisha kuna usalama kwa watu wake.
Licha ya sifa hizo Bwana Sharon anachukiwa sana na waarabu hasa wapalestina kwa dhuluma alizowatendea chini ya utawala wake.
Kiongozi huyo aliaga dunia siku ya Jumamaosi akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa takriban miaka minane.
Atazikwa baadaye leo katika shamba la familia yake jangwani Negev.
Maelfu ya waombolezaji walitoa heshima zao za mwisho kwa Sharon siku ya Jumapili wakati ambapo mwili wake ulikuwa umelazwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget