Bob Marley
Robert Nesta "Bob" Marley (6 Februari 1945 - 11 kutoka Mei 1981) alikuwa mwimbaji na
mwanamuziki muhimu nchini Jamaika. Alivuma hasa kunako
miaka ya 1970 na 1980. Ameweza kuifanya staili ya muziki wa reggae kuwa maarufu sana
duniani. Muziki wake mwingi ulikuwa unazungumzia hadithi za nyumbani kwake na
dini ya Rastafari ambayo yeye alikuwa
anaifuata. Kuna baadhi ya nyimbo zake zinahusu masuala ya dini na zingine
siasa.
Bob Marley alizaliwa na mama mweusi kijana
aliyeitwa Cedella Booker na baba wa Kizungu aliyeitwa Norvall Marley. Wakati
yungali bwana mdogo, marafiki zake walimpa jina la utani kama "Tuff
Gong".[1]Ameanza kazi zake za
muziki kunako miaka ya 1960 hivi akiwa na kundi lake la kina Wailing Wailers,
ambalo alilianzisha akiwa na marafiki wawili, Peter Tosh na Bunny Wailer. Mwaka wa 1962, Bob
Marley na kina Wailing Wailers wakafanikiwa kurekodi nyimbo zao mbili za kwanza
zilizoitwa "Judge Not" na "One Cup of Coffee".
Bob amemwoa Bi. Rita Anderson mnamo 1966 na
akajiunga na kundi akiwa kama mwitikiaji. Kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto
watano. Mmoja kati ya hao ni Ziggy Marley, ambaye pia ni mwimbaji
wa reggae maarufu sana.
- Mwaka wa 1974, kundi la Wailers likavunjika kwa sababu wanachama wote
watatu walitaka kujiendeleza kila mtu awe msanii wa kujitegemea. Lakini,
Bob Marley aliendelea kuita bendi yake jina la Bob Marley and the Wailers
na kujiunga upya na wanachama wapya na kuindelea kupiga muziki kama
kawaida. Mwaka wa 1975, Bob Marley akatoa kibao chake cha kwanza
kilichovuma kimataifa na kiliitwa "No Woman No Cry". HukoJamaika,
huhesabiwa kama kama shujaa wa jadi.
Post a Comment