http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Kuhusu Ashley Young na Manchester United


Ashley-Young3
Klabu ya Manchester United imetajwa kuwa tayari kusikiliza ofa mbalimbali ziotakazokuja kwa ajili ya winga Ashley Young baada ya mchezaji huyu kushindwa kumridhisha kocha wa United David Moyes ambapo Ashley amekuwa kwenye kiwango cha chini tangu msimu huu ulipoanza na amekuwa moja ya watu wanaolalamikiwa sana na mashabiki wa United kwa kuonyesha kiwango cha chini.
Zaidi ya hapo kocha wa United David Moyes anaonekana kukerwa na tabia ya winga huyu ya kujiangushaangusha akiwadanganya waamuzi ili wampe penalty kama ilivyokuwa kwenye mchezo kati ya United na Crystal Palaca mapema msimu huu.
Manchester United inatarajiwa kufanya usajili mwezi January lakini mpango huo pia utahusisha baadhi ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuondoka United ambao orodha yake pia inamjumuisha kiungo wa Japan Shinji Kagawa ambae ameshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza tangu David Moyes alipoanza kazi kama kocha wa United.
David Moyes 

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget