http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

LIGI KUU VODACOM: SIMBA YASHINDA, YANGA, AZAM ZALAZIMISHWA SARE!!

Saturday, 14 September 2013 20:47
Jumamosi Septemba 14
Simba 2 Mtibwa Sugar 0
Coastal Union v Prisons
Ruvu Shootings v Mgambo JKT
JKT Oljoro 1 Rhino Rangers 1
Mbeya City 1 Yanga 1
Kagera Sugar 1 Azam FC 1
Ashanti United v JKT Ruvu

LIGI KUU VODACOM leo ilikuwa dimbani na Mabingwa Watetezi Yanga walikuwa huko Uwanja wa Sokoine Mbeya na kutoka Sare ya Bao 1-1 na Timu ngumu ya Mbeya Cement, wenzao Simba walikuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuichapa Mtibwa Sugar Bao 2-0 na huko Kaitaba Mjini Bukoba Kagera Sugar ilitoka Sare Bao 1-1 na Azam FC.
Huko Mbeya, Wenyeji Mbeya City walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 49 alilofunga Bwigane Yeya na Didier Kavumbagu kuisawazishia Yanga katika Dakika ya 71.
Azam Fc nao waliponea chupuchupu baada ya kutanguliwa na Kagera Sugar kwa Bao la Themi Felix katika Dakika ya 25 na Khamis Mcha kurudisha katika Dakika ya 55.
Kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Simba waliipigiga Mtibwa Sugar kwa Bao za Henry Joseph Dakika ya 67 na Betram Mombeki Dakika ya 89
VIKOSI:
SIMBA: Abel Dhaira, Nassor Masoud, Issa Rashid, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Twaha Ibrahim, Said Hamis, Amisi Tambwe, Amri Kiemba, Haruni Chanongo.
Akiba: Abuu Hashim, Miraji Adam, Henry Joseph, Ramadhan Singano 'Messi', Betram Mwombeki, Abdulhalim Humud na Adeyum Ahmed.
MTIBWA SUGAR: Hussein Sharrif, Hassan Ramadhan, Paul George, Dickson Mbeikya, Salim Abdallah, Shaaban Nditi, Ally Shomari, Masoud Mohamed, Juma Liuzio, Shabani Kisiga, Vincent Barnabas.
Akiba: Said Mohamed, Ally Ally, Musa Hassan, Abdallah Juma, Awadh Juma, Salum Sued, Said Mkopi.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget