ARSENAL,
matumaini ya mwisho ya England kuikomboa Nchi hiyo balaa la kutokuwa na
hata Timu moja kwenye Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu
Msimu wa 1995/6, leo Usiku wanatinga Allianz Arena Jijini Munich kuivaa
Bayern Munich wakitakiwa kugeuza kipigo cha Bao 3-1 walichopewa katika
Mechi ya kwanza ili wao kusonga mbele.
RATIBA:
-Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal [3-1]
Malaga v FC Porto [0-1]
Lakini kazi hiyo kwa Arsenal ni ngumu
sana na ugumu umeongezeka baada ya taarifa za kuumia kwa Kiungo wao
tegemezi Jack Wilshere ambae atakuwa nje kwa Wiki 3 baada ya kuumia
enka.
Pia Arsenal itamkosa Straika wao Lukas Podolski, alieumia enka, na Kipa Wojciech Szczesny ambae amepumzishwa.
Lakini kwenye Kikosi cha Wachezaji 18
walioenda Germany wamo Lukasz Fabianski, Abou Diaby, Andrey Arshavin na
Kieran Gibbs ambao hivi karibuni walikuwa wakikosekana Kikosini.
KIKOSI CHA ARSENAL SAFARINI MUNICH:
Fabianski, Mannone, Jenkinson,
Mertesacker, Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Arteta, Coquelin, Ramsey,
Diaby, Oxlade-Chamberlain, Rosicky, Cazorla, Walcott, Giroud, Gervinho,
Arshavin
Arsenal hawataweza kumtumia Nacho Monreal kwa sababu alishaichezea Malaga hatua za Makundi ya UCL.
Huko Kambini Bayern Munich zipo habari
kuwa Bayern Munich itawakosa Franck Ribbery, alieumia, Arjen Robbens,
mwenye maumivu, pamoja na Schweinsteiger na Beki Jerome Boateng ambao
wako Kifungoni.
Pia, Bayern haitakuwa na majeruhi wa muda mrefu Beki Holger Badstuber ambae atakuwa nje Msimu wote.
VIKOSI VINATARAJIWA:
BAYERN MUNICH:
Manuel Neuer, Philipp Lahm, Daniel Van Buyten, Dante, David Alaba,
Javier Martinez, Luiz Gustavo, Thomas Muller, Toni Kroos, Xherdan
Shaqiri, Mario Mandzukic.
ARSENAL: Lukasz
Fabianski, Bacary Sagna, Per Mertesacker, Laurent Koscieln, Thomas
Vermaelen, Abou Diaby, Theo Walcott, Santi Cazorla, Mikel Arteta,
Olivier Girou, Gervinho.
MALAGA V FC PORTO [Mechi ya kwanza 0-1]
Kocha wa Malaga Manuel Pellegrini
amepatwa na wasiwasi kwa kuzagaa taarifa kuwa hii ndio Mechi kubwa
kabisa katika historia ya Klabu hiyo wakiwania kupindua kipigo cha Bao
1-0 walichopewa na FC Porto huko Ureno katika Mechi ya kwanza na amekuwa
na hofu hilo litaathiri Saikolojia ya Timu yake.
Huko Jijini Malaga kumekuwa na
shamrashamra Msimu wote huu kwa kuiona Timu yao ikicheza kwa mara ya
kwanza kwenye UCL na tena bila kufungwa katika Mechi zake zote za UCL
Msimu huu hadi walipochapwa na FC Porto.
Ukubwa wa Mechi hii kwa Malaga
umeongezeka maradufu kwao baada ya UEFA kuwafungia kucheza Ulaya kwa
Misimu minne kuanzia Msimu ujao kwa kushindwa kulipa Madeni yao kwa
Wachezaji na Wadau wengine.
Kwa sasa Malaga wako nafasi ya 4 kwenye La Liga wakiwa nyuma ya Vinara Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid.
ROBO FAINALI:
Mechi ya 1=Tarehe 2 na 3 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 9 na 10 Aprili 2013
NUSU FAINALI
Mechi ya 1= Tarehe 23 na 24 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 30 Aprili na 1 Mei 2013
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, London.
Post a Comment