>> MECHI YA SIMBA, COASTAL WATAZAMAJI 6,284, YAINGIZA MIL 37/-
>> UCHAGUZI TAFCA KUFANYIKA MOROGORO JUMAMOSI!!
SOMA TAARIFA KAMILI:
Release No. 043
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi 12, 2013
LIGI YA VODACOM KUENDELEA J’MOSI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea Jumamosi (Machi 16, 2013) kwa mechi
tatu zitakazochezwa katika miji ya Mwanza, Dar es Salaam na Manungu,
Turiani mkoani Morogoro.
Toto Africans inayopigana kukwepa kurudi
daraja la kwanza itakuwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kutoka Tanga
katika mechi itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Vinara wa ligi hiyo Yanga wataumana na
Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Manungu utakuwa
mwenyeji wa mechi ya Mtibwa Sugar na Coastal Union.
UCHAGUZI TAFCA KUFANYIKA MOROGORO
Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha
Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Machi 16
mwaka huu) mjini Dodoma ambapo wajumbe wanatakiwa kuripoti siku moja
kabla ya uchaguzi.
Wagombea waliopitishwa kuwania uongozi
na Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya uenyekiti wa Ramadhan Mambosasa
ni Oscar Don Koroso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti) na
Katibu (Michael Bundala).
Wengine ni Gabriel Gunda (Katibu
Msaidizi), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania- TFF (Wilfred Kidao) wakati wagombea ujumbe wa Kamati ya
Utendaji ni Jemedali Saidi, George Komba na Magoma Rugora.
KIM KUTAJA KIKOSI CHA KUIKABILI MOROCCO
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars), Kim Poulsen anatarajia kesho (Machi 13 mwaka huu) kutaja
kikosi chake kitakachoivaa Morocco.
Mkutano huo wa Waandishi wa Habari
utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
itacheza na Morocco kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 24
mwaka huu.
MECHI YA SIMBA, COASTAL YAINGIZA MIL 37/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya
Simba na Coastal Union iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 36,820,000 kutoka na watazamaji 6,284.
Viingilio katika mechi hiyo namba 138
iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 vilikuwa sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo
wa sh. 8,265,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
ni sh. 5,616,610.17.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 4,202,924.97, tiketi sh. 3,183,890, gharama za
mechi sh. 2,521,754.98, Kamati ya Ligi sh. 2,521,754.98, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,260,877.49 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 980,682.49.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment